10/05/2010

Mtazamo wa Kitogo juu ya Tanzania ya 2020

Mwendesha libeneke la http://varsitycollegetz.ning.com, Kitogo anasema akiiangalia Tanzania ya 2020 anaiona ni Tanzania hii hii, na ana haya ya kusema;

Mambo mengi yananifanya nisione dalili za mabadiliko ya kiuchumi na kimaendeleo nchini kwetu Tanzania kwa mfano:

- Hakuna mipango madhubuti ya kimaendeleo
- Hata ile mipango michache ya kimaendeleo inayowekwa haitekelezwi angalia; mabasi ya kasi, vitambulisho, kilimo kwanza, upunguzaji wa matumizi ya serikali, udumishwaji wa elimu, hali bora za wafanyakazi, kuvutia uwekezaji (angalia utendaji bandari na shirika la ndege, mamlaka ya kodi), n.k
- Hakuna wito wa kisiasa kwa karibu wanasiasa wote
- Rushwa kila mahala (nilishawahi kuvamiwa na kuibiwa bongo nilipoenda polisi nikaombwa rushwa ili tatizo langu lishughulikiwe - so nikawa nimeibiwa mara 2).
- Viongozi wamekuwa watemi zaidi kuliko watendaji. Mfano ni juzi tu Mkulu alivyowakoromea wapiga kura (wajenga nchi) wafanyakazi.
- Viongozi wanachaguliwa kwa kujuana na umaarufu na si sifa za kiutendaji
- Mambo ya msingi hayatiliwi maanani ukilinganisha na yale yasiyo na msingi - Vipi taifa litaendelea bila ya kuwa na wasomi? mbona elimu haipewi kipaumbele inayostahili? miundo mbinu je? pembejeo za kilimo?
- n.k

Kwa sababu hizo juu na nyingine kadhaa sioni kama Tanzania itapiga hatua kwa siku zijazo. Labda kutokee mabadiliko makubwa.

Wadau tunasemaje juu ya mtazamo wa mwenzetu?

2 comments:

  1. ...mipango itatoka wapi kama mwenyekiti wa kijiji anakuja kutoa lugha ya kimabavu kwa watu walio sehemu ya mikakati kitija?

    ni swali tu!

    ReplyDelete
  2. Tusikate tamaa. Tuchukue hatua za kupindua yaliyopo. Inawezekana.

    ReplyDelete