19/11/2010

Jamani "Kunradhi Kitumbua si Andazi"

Usafiri wetu wa kwenda nyikani kuna kipindi unaleta mushkeri

Baada ya kutoonekana kitambo kidogo hapa kibarazani (takribani miezi mitano na ushee hivi...), nimerejea tena. Nilikuwa huko nyikani na mawasiliano yalikuwa tata vilivyo. Sikuwaaga lakini waswahili wanasema "kunradhi", ndugu zangu kukosekana kwangu kuliambatana na mambo mengi huko. Mengine nimeyakusanya nitakuwa nawarushia moja baada ya jingine kadri tunavyoendelea kubarizi kibarazani, nimefurahi kurudi tena!

2 comments:

  1. Karibu, karibu, Karibu saannaaaaaaaaaaaaaaaa kaka M. Yaani we acha tu jinsi ulivyokuwa unatamaniwa. Karibu kaka na tunasubiri sana haya uliyokuja nayo:-)

    ReplyDelete