12/04/2011

Hepibesidei Mdau Joe!

 Joe

Leo mdau Joseph Abril Andabwa Jackson,almaarufu "Joe", rafiki mkubwa wa Mwanasosholojia toka enzi zileeee za utotoni, anakumbuka siku yake ya kuzaliwa. Kibaraza hiki kinampongeza sana kwa kukata mwaka mwingine katika siku zake alizojaliwa na Rabuka kuishi, na kinamtakia maisha marefu zaidi yenye baraka na mafanikio.

Picha hii ilipigwa mwaka 2009 wakati mdau Joe alipofanya ziara pamoja na Mwanasosholojia katika misitu ya Amani, Tanga hiki ni kibao cha mashine ya kusaga nafaka inayoendeshwa kwa nguvu ya maji iliyopo katika kijiji cha Kisiwani, Amani
Mdau Joe (mwenye jacket na suruali ya jeans,wa pili kushoto) akiangalia usagishaji nafaka katika mashine hiyo
Mdau Joe akiwa amepozi mbele ya moja ya majengo ya mamlaka ya misitu ya Amani, kijiji cha Kisiwani. Jengo hilo lilijengwa na Wajerumani enzi za ukoloni
Mdau Joe akiwa amekula pozi. Nyuma yake inaonekana misitu adhimu ya Amani, sehemu ya wilaya ya Muheza, mkoani Tanga.

1 comment: