19/05/2011

Hii ya Mwisho wa Dunia Imekaaje?

Kundi la wahubiri wakizunguka mitaani New York, kuieleza dunia juu ya mwisho wake Jumamosi ya tarehe 21 mwezi huu.

Bwana Osvaldo Colon naye akiwa miongoni mwa wahubiri wa mwisho wa dunia
Kumekuwa na maoni tofauti na mkanganyiko juu ya hawa wenzetu wahubiri huko New York, Marekani, wanaotangaza kuwa Jumamosi ya tarehe 21 mwaka huu (yaani keshokutwa tu), ndio utakuwa siku ya hukumu na mwisho wa dunia.

Hili ni suala la kiimani zaidi ambalo tafsiri yake pia inategemea na jinsi ambavyo linachukuliwa. Ndugu zetu hawa wanatumia mahesabu kutoka katika biblia na wametawanya matangazo mengi huko New York na maeneo mengine duniani, na wanasema kuwa katika kitabu cha ufunuo imeandikwa kuwa kutakuwa na tetemeko kuu dunia nzima siku hiyo. 

Wanatahadharisha kuwa haiyumkini lisitokee kwa wakati mmoja duniani kote kutokana na kutofautiana masaa, lakini hali hiyo itatokea tarehe 21 mwezi huu. Jambo hili ambalo pia liliwahi kutabiriwa miaka kadhaa nyuma (lakini halikutokea), kwa sasa linakuzwa zaidi na Harold Camping, ambaye ni Rais wa Redio ya Familia (Family Radio), inayotangaza kutokea California, Marekani. Kulifahamu hili zaidi ngonga hapa

Ninajiuliza maswali kadhaa juu ya suala hili. Limekwisha sababisha mahangaiko kiasi gani kwa watu mbalimbali duniani?Kama nilivyosema awali, ni suala la kiimani, lakini wale wasio "waumini" wa mahubiri haya, nao pia wana hali gani kwa sasa? Maswali hayaishi, yanaendelea na kuendelea, lakini labda kikubwa nafikiri ni kusubiri na kuona kitakachotokea (kama kweli kitatokea). Sijui wewe mdau unaona hii imekaaje?

1 comment:

 1. Hii ya mwisho wa dunia mimi binafsi
  sikubaliani nayo haijaka vizuri japo nakubali ya kwamba kuna mwisho wa dunia,
  navyoamini mwisho wa dunia hakuna ajuaye ila muumba wa mbingu na ardhi na vilivyomo.
  Dalili ambazo zimeelezwa katika vitabu vitukufu vya mungu zimeshaanza kuonekana na zingine bado hazijadhihiri hivyo kwa yeye kutabiri hivyo kwa muono wangu yeye
  ndio kati ya moja ya dalili zilizoelezwa katika vitabu vya mungu ya kuwa watakuja manabii wa uongo ndio kama hao wanaanza
  kuonekana na kuzungumza katika vyombo vya habari.Ni hayo tu.
  Ally Shaaban

  ReplyDelete