16/05/2011

Jumatatu kama ya Leo 2022

Nimekutana na hii sehemu, nikajikuta nacheka kidogo na kutafakari, nikaona si vibaya kama nikaipachika hapa kibarazani...

 Eeeh!!!
Hivi umeshawahi kukaa na kufikiri miaka michache ijayo mambo yatakuwaje??? Hebu kwa mfano mwaka 2022 twaweza shuhudia yafuatayo hapa Tanzania.

1. Wakati huo dawa ya ukimwi ishapatikana, mtu unaenda ofisini baada ya kutokuwepo kwa takribani majuma mawili. Bila shida unaongea na bosi wako huku ukimueleza..."Bosi, yaani ka-ukimwi kalinitandika vibaya sana last week" halafu sijui kwa nini mimi kananiandama hivyo.......

2. Bungeni napo tunakuwa na waheshimiwa kama Mr Ebo, Kingwendu, Bambo na wafananao na hao. Unasikia spika akisema....Mheshimiwa Bambo swali la nyongeza. Bambo: "Mheshimiwa spiko pamoja na majibu mazuri ya Waziri wa michezo na utamaduni naombi kuulizi swali hivi kwa nini siku ya fiesto isiwe sherehe ya kitaifo ambapo raiso atatoa mapumziko nchi nzimooo???
 
3. Uswahilini nako kama Manzese kutakuwa na maghorofa ya nguvu...Majungu ya akina mama wa apartment zilizo jirani yatakuwa...House girl wangu siku hizi hapiki bila kutizama DSTV ili kuona wenzake wa Afrika Kusini wanavyotengeneza masalo. Wewe wako bado anatizama kipindi ya mapishi ya ITV na Clouds TV???? Tv ya Clouds wakati huo kama CNN.

 4. Nako maofisini itakuwa utata mtupu, haitokuwa jambo la ajabu kuongea na bosi wa kiume huku hereni zinamning'inia masikioni. Na si ajabu akipata taarifa ya ghafla kuwa kampuni yake imepata hasara suruali ikamdondoka manake uvaaji ni ule wa bila mkanda huku ikiwa imeegeshwa chini ya matako (kata-K)"au nusu mlingoti".

5. Ukipita Sinza ndo utatoa macho...watoto wa chekechea wamajipanga kwenye ATM machines kuchukua pesa ya kununulia lambalamba shuleni kwao. Yaani itakuwa mtafaruku mtupu...Mara mtoto mmoja anamwambia mtoto mwenzie, baba kanidipositia cheki  feki, imebaunsi hivyo leo ice cream nitachukua kwa overdraft.

1 comment:

  1. Ilikuja ndui ikatufanya mbaya, baadaye ikapatiwa ufumbuzi, sasa ukimwi, ...nahisi ikitoka hiyo litakuja bab kubwa, kama hatutajirebisha, siombei, ila...kauli zinaogopesha!

    ReplyDelete