09/05/2011

Mh.Tundu Lissu apata Nishani!

Mh. Tundu Antiphas Lissu
Tarehe 6 Mei 2011, Chuo Kikuu cha Bridgeport kilichopo mji wa Bridgeport, Jimbo la Connecticut nchini Marekani kimemtunuku nishani ya 'Mwenza wa Heshima wa Chuo cha Kimataifa cha Chuo Kikuu cha Bridgeport' (Honorary Fellow of the International College). Citation ya nishani hii inasomeka kwamba ...Mheshimiwa Tundu Antiphas Lissu cheo cha Mwenza wa Heshima wa Chuo cha Kimataifa kwa kutambua utumishi wake uliotukuka katika kuendeleza haki za binadamu, ujenzi wa demokrasia na ulinzi wa mazingira katika Tanzania na Afrika... Kwa Kiingereza: ...In recognition of his  inspired service for the furtherance of human rights, democratic institutions and the protection of the environment in Tanzania and in Africa...

Tuzo hii imekabidhiwa kwake na Mkuu wa Chuo cha Kimataifa Dr. Thomas J. Ward na Rais wa Chuo Kikuu cha Bridgeport Dr. Neil Albert Salonen.

Sehemu ya Jengo la Maktaba la Chuo Kikuu cha Bridgeport

 Kibaraza hiki kinachukua nafasi hii kumpongeza sana Mheshimiwa Tundu Lissu kwa nishani hii, ambayo ni kielelezo tosha cha jamii ya wanataaluma kutambua mchango wake katika jamii. Kaza buti pasi hofu wala shaka yoyote Mheshimiwa Lissu.


2 comments:

  1. Ni kazi yetu nasi kuwatafuta ma mia ya Tundu Lissu wengine wasieonekana kirahisi katika jammi zetu. Na wako wengi sana!


    Kama Mwafrika nami nimefurahi sana, kwani demokrasia nikiini cha ustaarabu!

    ReplyDelete