22/05/2011

Ni Jumapili, bado tunavuta pumzi!

Harold Camping
Yep, ni Jumapili sasa, Jumapili ya tarehe 22 Mei. Ile Jumamosi ya tarehe 21 Mei ambayo mzee wetu, Mhandisi mstaafu, Mchungaji na Kiongozi wa Redio ya Familia, Harold Camping alisisitiza kuwa ndio ungekuwa mwisho wa dunia, imeshapita. Lengo si kushangilia hapa, lakini ni kutamka tu kuwa bado tunaendelea kuvuta pumzi, na labda kuendelea kushuhudia vituko mbalimbali vijavyo vya duniani. 

Utabiri wa Camping ulivuta hisia za maelfu ya watu katika nchi mbalimbali duniani. Kiasi kwamba wengine walishauza hata mali zao, wakisubiri tu temeteko lililotabiriwa na hatimaye kwa walio haki kunyakuliwa na Kristu. Hii ni mara ya pili kwa utabiri wa aina hii wa mzee Camping, kufuatia ule wa mwaka 1994. Sijui nini safari hii kitatokea kwake, lakini tayari baadhi ya watu wameshaanza kumrushia shutuma nzito na kumkejeli, wengine wakisema si ajabu kwa yeye kutabiri haya kutokana na kusumbuliwa na uzee. Camping ana umri wa miaka 89 sasa. Binafsi amenikumbusha pia yule Mchungaji maarufu kule Uganda, kipindi fulani, Bwana Kibwetere. Mambo ya imani haya jamani.

5 comments:

  1. Haswaaaa haya ni mambo ya IMANI. Unajua ukiamini kila wasemalo watu katika dunia hii hutaishi kabisa...Kwa mfano haya mambo ya chakula, maana kila chakula hasa kwa ughaibuni ukila hiki wanasema utanenepa usile nk nk. ......

    ReplyDelete
  2. Nasikia pia WAFU hawajisiki kuwa wamekufa! Kwa hiyo labda tuandikayo hapa tukijifikiria tuko hai ,...
    ... ndio marehemu wajisikiavyo kwa hiyo labda waliohai duniani washalia sana tu au tu Adam na Eva wao ndio kwanza hata tunda hawajala!:-(

    ReplyDelete
  3. @Mtakatifu...mmmh!lakini kuna atamaniye kufa (ukiacha wakatao tamaa na maisha na kuona suluhisho ni kufa..?), nawaza tu kwa maandishi..lol!

    ReplyDelete
  4. @Mats: Nasikia memba wa alqaida ni fulu kujiua hata kabla maisha hayajawakatisha tamaa kwa kuwa kirahisi ukifa na hamu zako mbinguni unagewa fulu mabikira lukuki!:-(

    ReplyDelete
  5. @Mtakatifu..nami nasikia hivyo, si hao tu hata fundamentalists wa dini wengine, hii dhana ya maisha baada ya kifo (life after death) imetafsiriwa tofauti tofauti kulingana na matakwa ya kiimani...sasa kuwaza kwangu kunapanuka...niliwasahau hawa :) teh!teh!

    ReplyDelete