24/05/2011

"Samahani" toka kwa Babu wa Mwisho wa Dunia

  
Mhubiri wa Marekani, babu Harold Camping aliyetangaza mwisho wa dunia kuwa ni Mei 21 mwaka huu, ameibuka na kuitaka radhi dunia na kusema sasa tarehe yenyewe hasa ya mwisho wa dunia itakuwa ni Oktoba 21 mwaka huu. Katika mahojiano yake na SkyNews babu Camping amesema yeye siyo "jiniaz" na kwamba siku zote anatafsiri biblia na kumuomba Mungu busara kabla ya kutamka kitu.

Kazi ipo...amesogeza mbele...nini kitafuata? Tutege masikio

2 comments:

 1. Haswaaa ..tutege masikia na pia tusifumbe macho...kaaaaazi kwelikweli.

  ReplyDelete
 2. Kwani huko Marekani hawapo madaktari wa kumtibu mgonjwa wa akili?


  Au anazo akili zake timamu ili tu hii ni namna kwake ya kutengeneza pesa kwa kuwatapeli wagonjwa wa akili kwa mahubiri potofu?


  Takwimu zasemaje kuhusu watu waliejiuwa; waliyeacha kunywa vidonge vya magonjwa yao na kisha wakafa; waliepoteza biashara zao; na waliyeacha kazi ghafla YOTE KUTOKANA NA UONGO WA HILI LIBABU HARIBIFU?


  Mbona Biblia ilisema kinaganaga kwamba hatujui siku wala saa atakapokuja Mwanakondoo?

  ReplyDelete