29/05/2011

Tuzo zasogezwa mbele!


Taarifa ya Tanzanian Blog Awards inasema kuwa...

Kutokana na maombi ya wengi ambayo tumeyapokea. Tumeongeza muda wa kupendekeza majina yatakaoshiriki katika mashindano yetu. Hivyo tarehe ya kutuma majina ya blog hizo umebadilishwa kutoka tarehe 31 May 2011 kwenda tarehe 10 June 2011.

Tunataka kuwaambia watu ukipost habari za tangazo letu tafadhali usikose kutwambia ili turudishe fadhila. Pia sasa hivi tumeamua logo ya shindano hili ni hii hapa...Kuna nyingine tulitengeneza mwanzoni lakini hii ndio tumeichagua kwa sasa. Sasa kama ukipost habari za shindano hili tafadhali tumia picha hii.

Pia kutokana na blog mbalimbali zimepost hili shindano letu na tumeona kuna maswali ambayo hayana majibu kwenye comments zao. Na sisi kwa vile hatutaweza kupitia kila blog iliyopost maelezo na kuwaelewesha watu. Hapa (kwenye www.tanzanianblogawards.com) nitaweka majibu ya maswali baadhi nimeona yameandika najua kuna mengi lakini hatujaweza kuyaona. Ila kama una swali usisite kututumia.

PENDEKEZA BLOG UZIPENDAZO NA BOFYA HAPA KWA TAARIFA ZAIDI

2 comments: