25/06/2011

Chagua Mwanasosholojia Tuzo za Blog!

Muda wa kuanza kupiga kura kwa ajili ya tuzo za Blogs umewadia. Lifuatalo ni tangazo kutoka kwa waandaaji likielekeza namna na taratibu za kupiga kura:

Kura zitaanza kupokelewa kwenye blog ya TANZANIAN BLOG AWARDS tarehe 25/06/2011 kuanzia saa 12.01AM (saa za Africa ya mashariki)  mpaka tarehe 09/07/2011 saa 11:59PM (tafadhali zingatia muda). Utaweza kupiga kura yako katika kipindi cha wiki mbili.  Tumeamua kuweka muda huo wa wiki mbili ili kuepusha malalamiko ya wale wanaopenda kulalamika tu kwa kila jambo. Tunategemea katika kipindi hicho kila mtu anayetaka kupiga kura ataweza kupiga kura na pia wenye blogs wataweza kuwaelekeza wasomaji wake wao wote waje hapa kupiga kura hizo.. 

Utaweza kupiga kura moja katika kila kipengele (category) kila baada ya masaa 12. Ingawaje tutaruhusu watu waweze kushare kwa email zao maelezo ya kura hizi kwa watu mbalimbali ili watu hao waweze kushiriki lakini ufahamu kuwa tutazuia watu kwa kutumia cookies na Ip address. Tunajua njia zote zina mapungufu yake lakini tunaamini kuwa watu hawataenda extra miles ili tu waweze kupiga kura zaidi ya mara moja katika kipindi hicho cha masaa 12.

Tunajua tukitumia tu cookies watu wengine wanaweza kudelete, au kutumia browser tofauti na kupiga tena kura na tukizua Ip address tu wenye kutumia dial up, au proxy servers kama anonymous nayo unaweza kupiga kura tena. Hivyo kutokana na sababu hizo tumeamua kutumia njia zote mbili. 


Hivyo kama utaona huwezi kupiga kura yako kutoka kwa network au computer fulani basi ufahamu kuwa kuna mtu ametumia hiyo computer au network kupiga kura yake. Subiri kwa masaa kadhaa na ujaribu tena.

  
Nadhani tumeelewana lakini kama kuna mtu ana swali lolote basi usisite kutuandikia.

Tanzanian Blog Awards Team 
Mdau wa kibaraza hiki, ingia HAPA kwenda sehemu ya kupigia kura katika Blog ya Tanzanian Blog Awards. Ukiingia, Blogs zote zinazoshindanishwa zimeorodheshwa kulia. Unapiga kura kwa "kukliki" kidude cha duara kinachoonekana kabla ya blog. Kibaraza chenu cha Mwanasosholojia kimeteuliwa katika tuzo zifuatazo: 
1.  Best Entrepreneur Blog
2. Best Informative - Economy Blog
3. Best Informative - Lifestyle Blog na
4. Best Inspiration Blog.

 Piga kura yako sasa mpaka tarehe 09/07/2011. Kibaraza kinatanguliza shukrani za dhati kwako mdau!

1 comment:

 1. Siamini kama kweli watu mmekazania upuuzi huu. Ukishinda ndiyo utapata nini? Umaarufu? Unawajua hawa waandaaji?

  Zoezi zima hili ni upuuzi mtupu. Watanzania hatuwezi kufanya kitu kwa haki na transparency. Kila kitu ni kwa kujuana na kufuata sifa na umaarufu.

  Bloggers wana nafasi kubwa sana katika jamii na wanapokubali kufanyiwa mchezo wa kipuuzi kama huu inasikitisha.

  Maswali ya msingi yaliulizwa kuhusu hawa waandaaji wa hizi awards na mpaka leo hawajulikani ni akina nani, lengo lao hasa ni nini na uteuzi huu ulifanyikaje. Ni nani wanaopiga kura? Maswali mengi sana ya msingi na ambayo hayakupata majibu yalishaulizwa hapa:

  http://changamotoyetu.blogspot.com/2011/05/tanzanian-blog-awardsmtazamo-na-msimamo.html

  Ni aibu kwamba mablogger wenye majina makubwa kama Michuzi na Mjengwa, mablogger ambao wanapaswa kuwa kielelezo nao wanakimbilia shindano hili lisilo na kichwa wala miguu. Umaarufu huu mnaoutafuta kwa hali na mali utawafikisha wapi?

  Blogu yangu ilipendekezwa sijui na nani lakini niliwaambia hawa waandaaji wasiojulikana waiondoe mara moja katika shindano hili la kipuuzi.

  Sasa nawe Mwanasosholojia umekazana kweli kweli ushinde. For what?

  ReplyDelete