16/06/2011

Miaka miwili, bado upo nasi

Leo imetimia miaka miwili kamili tokea ututoke mama yetu mpendwa, Magreth Mabula-Senga. Haupo nasi kimwili baada ya kukuzika kule makaburini Yombo, Dar es Salaam, lakini kiroho mama, upo nasi siku zote. 

Mama, tunakukumbuka kila saa, tunakumbuka upole wako, busara zako, uvumilivu wako, lakini zaidi upendo wako wa pekee ambao umefanya tuweze kufika hapa tulipofika. Mama ulitaka tuishi maisha ya mafanikio, maisha ya upendo kama uliokuwa nao, maisha ya kusaidiana. Tunakumbuka mama kuna kipindi ulilazimika hata kujinyima kwa ajili yetu sisi! Kuna kipindi mama ulitoa machozi ulipoona mambo kwa upande wetu hayaendi sawa. Kwa hakika mama ulitupenda sana sisi wanao.

Mama, tulipenda uendelee kuwepo. Ndio maana hata ulipopatwa na maradhi na kulazwa hospitali, tulikuwa na wewe karibu, tukihangaika na kukuombea Mungu akuponye na kuendelea kukupa pumzi. Lakini haikuwa hivyo, kwa mapenzi yake muumba, mama ulituacha kimwili. Ilikuwa ni pigo kubwa sana kwetu na hatukuwa na namna au uwezo wa kulizuia hili. Tulikubali na kuhuzunika sana.


Tunakuahidi mama yetu, tutazidi kuyaishi yale ambayo uliyapenda huku tukiomba kila wakati Mwenyezi Mungu azidi kutukarimu moyo kama uliokuwa nao. Tunazidi kukuombea mama yetu, roho yako istarehe kwa amani. Tunaomba na wewe utuombee, tuweze kupata baraka na mafanikio leo na siku zote zijazo. 

MAMA TUNAKUPENDA SANA. NI MIAKA MIWILI SASA LAKINI BADO UPO NASI

8 comments:

 1. Ustarehe kwa amani mama yetu tutakukumbuka milele!!

  ReplyDelete
 2. Poleni sana kwa kuondokewa na mama kipenzi chenu,Hatuna budi kumshukuru Mungu kwa kila jambo.Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe Milele Amina!.Mungu awatie nguvu daima.

  ReplyDelete
 3. Pole sana kaka,Mwenyenzi Mungu ailaze roho ya mama mahala pema peponi,Amen

  ReplyDelete
 4. POLE SANA NDUGU YANGU MWANASOSHOLOJIA.SIE TULIMPENDA MAMA LAKINI BWANA ALIMPENDA ZAIDI,NA KWA VILE NI MWENYE UPENDO BASI ANAMPATIA PUMZIKO NA MWANGA WA MILELE.NAUNGANA NA WEWE BINAFSI NA FAMILIA YAKO KATIKA MAOMBOLEZO HAYA...http://www.chahali.com/2011/06/kumbukumbu-ya-miaka-miwili-ya-kifo-cha.html

  ReplyDelete
 5. Ahsanteni sana ndugu zangu!Sina cha kuelezea shukrani zangu na upendo wenu kwetu. Mungu awabariki sana.

  ReplyDelete
 6. Kaka pole sana kuondokewa na Mama wanasema Mungu alitoa na Mungu ametwaa, kazi yake haina makosa.Ni wazi mlimpenda sana ila Mungu kampenda zaidi.Mungu awape nguvu wewe na familia yenu RIP mama Magreth.

  ReplyDelete
 7. ANGELA JULIUS05/10/2011, 09:49

  POLENI SANA KWA PIGO KUBWA LILILOIPATA FAMILIA KWA KUONDOKEWA NA MAMA MPENDWA,KIKUBWA NI KUMWOMBEA PUMZIKO ZURI LA MILELE NA ATUOMBEE HUKO ALIPO INGAWA KIMWILI HATUPO NAYE ILA KIROHO TUPO NAWE MAMA, PUMZIKA PEMA PEPONI MAMA AMEIN.

  ReplyDelete