18/06/2011

Toronto wakumbuka waliouawa North Mara

Watu wapatao sabini walikusanyika nje ya Chuo Kikuu cha Toronto, Munk School of Global Affairs kwa ajili ya kumbukumbu ya mauaji ya raia saba yaliyotokea mapema mwaka huu katika Mgodi wa dhahabu wa North Mara, unaomilikiwa na kampuni ya Barick Gold. 
Suala la mauaji haya lilichukua nafasi katika vyombo mbalimbali vya habari vikiwemo vya nchini Canada, na kusababisha msuguano mkubwa kati ya Polisi na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Tukiacha suala la siasa pembeni, mauaji ya raia hawa sio tu yameacha pengo kubwa kwa familia zao, lakini pia yameacha doa kubwa na kielelezo cha matumizi yaliyozidi ya nguvu za dola kwa raia. Kibaraza hiki kinawapongeza watu hawa waliochukua jukumu la kuwakumbuka raia waliouawa kwa njia hii. Wakati sasa umefika wa vyombo vya dola kuangalia namna ya kulinda usalama wa raia na mali zao pasipo kusababisha madhara kama haya.

Kupata taarifa zaidi za kumbukumbu hii, tembelea HAPA na HAPA na HAPA

1 comment: