10/02/2012

Vunja Mbavu

Kunradhi kwa wana-kibaraza kwa ukimya wa kitambo ulioambatana na mambo lukuki. Leo nimekutana na vunja mbavu hii kutoka katika ukurasa wa mwana-kibaraza mwenzetu Adam Kaombwe...


Jamaa watatu walikuwa wakisafiri kupitia kwenye msitu mnene na kwa bahati
mbaya wakakutana na majitu yanayokula watu na yakawakamata. 
Yale majitu
yakawaambia 'sisi tuna mtihani ambao ukifaulu tunakuacha uende zako, la
ukishindwa unaliwa.'
Basi yale majitu yakawatuma msituni wakiwa chini ya
ulinzi kukusanya kila mmoja wao matunda kumi ya mti watakaochagua.
Baada ya
muda mfupi mmoja wao akawa amefanikiwa kurudi na matunda aina ya Apple.
Akaambiwa mtihani mlionao ni kuhakikisha kuwa unakula matunda yote kumi kwa
kumeza bila kutafuna, moja moja lakini usionyeshe hisia yeyote katika uso
wako.
Yule aliyekuja na apple akaogopa mno lakini akajizuia kuonyesha hofu
yake, wakati huo huo yule wa pili akawa anakuja na matunda yake mkononi aina
ya rasberry ambayo ni madogo na hayana kokwa. 
Yule wa kwanza alipoweka apple
mdomoni kwake lilimzidi kinywa na hivyo akagugumia maumivu kwa hiyo akaliwa
mara moja.
Huyu wa pili kuona hivyo akazuia hisia zake za hofu kubwa na
akapewa mtihani ule ule wa kula matunda hayo moja baada ya jingine. 
Kutokana
na udogo wa matunda hayo na kuwa hayana kokwa ndani alikula bila matatizo
mpaka tunda la tisa.
Alipofika tunda la tisa akaangua kicheko kikubwa mno kwa
ghafla hivyo na yeye akaliwa mara moja.Mara wakajikuta wako ahera yule wa
kwanza na wa pili. 
Yule wa wa kwanza akashangaa sana na kumuuliza 'imekuwaje
wewe umeshindwa kula vile vijitunda vyote na ukaanza kucheka?' 
Huyu wa pili
akajibu na kusema ' nilimwona jamaa yetu wa tatu akija na mananasi'

No comments:

Post a Comment