Kuna kipindi naumia
Maumivu kugugumia
Unapopatwa na udhia
Hata uanzapo kulia
Nashikwa na huzuni
Nayo majonzi moyoni
Pia raha siioni
Nikikutazama usoni
Ni mimi nakukwaza
Kujisahau kuwaza
Kutofikiria kwanza
Kudhani nakuliwaza
Ni kawaida kwa wawili
Kupishana Kiswahili
Twapendana kweli kweli
Makwazo tuyastahimili
Wewe ni mzuri mno
Unanipa penzi nono
Wanilaza kama pono
Unipapasapo kwa mikono
Kukukwaza sitamani
Si kusudi asilani
Ewe wangu mwandani
Nielewe jamani
Siku zote nakuahidi
Moyo wangu ni shahidi
Sitakuja kukukaidi
Penzi langu ufaidi
Nisogelee mwandani
Na unilaze kifuani
Ninong’oneze sikioni
Na kunibusu shingoni
Ya mapenzi nayo ni MAKUBWA!
ReplyDeleteMkuu kumbe unaimudu fani ya malenga wetu (unakikumbuka kipindi hicho huko Radio Tanzania?)
ReplyDelete@ Mkuu Chahali...:)
ReplyDelete